Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, wakati anaongea na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba27,2024.
“Vituo Vya kupigia kura vimeongezwa ili viweze kuwafikia wananchi wote zoezi la kupiga kura litaanza kuanzia saa2-10 jioni kwa wale waliokwisha panga foleni na atakayefika zaidi ya saa10 jioni hatakuwa na nafasi ya kupiga kura”, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Chalamila anasema kwa yeyote atakayejaribu kuharibu amani katika uchaguzi atachukuliwa hatua Kali.
“Hakutakuwa na mtu yeyote atajaribu kuharibu amani iliyopo akaachwa salama, tutamnyakua na kuwaacha walio na Nia ya kuchagua viongozi wa Serikali ya Mtaa”, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Nao baadhi ya wananchi wanaelezea watakavyoshiriki Uchaguzi huo.
“Nimejiandaa kushiriki kwa sababu nilijiandikisha na nitapiga kura, na vigezo Vya kuchagua kiongozi nitaangalia mwenye sera nzuri za kutuvusha”, Norah Prosper, Mkazi wa Mkuranga.
“Nimejiandaa vizuri kupiga kura, na Nina imani viongozi nitakaochagua watatuvusha kwenye changamoto zinazotukabili “, Ivan Frank, Mkazi wa Dar es Salaam.
“Kikubwa nachokiomba ni uchaguzi huru na wa haki na kuwe na amani na utulivu katika kipindi chote cha zoezi la kupiga kura”, Franklin Sanjawa, Mkazi wa Dar eś Salaam.