Jumanne , 12th Nov , 2024

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini, imefanikiwa kukamata kilogramu 1066 za dawa za kulevya na mililita 447 za dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuteketeza ekari 157 za mashamba ya bangi na lita 19,804 za kemikali bashirifu pamoja na kuwakamata watu 58.

Aretas Lyimo Kamishna Jenerali DCEA.

Akiongea na waandishi wa habari kamishna jenerali wa mamlaka hiyo Aretas Lyimo anasema kupitia chunguzi walizofanya wamegundua wanawake wanaongoza katika matumizi ya Skanka.
"Kati ya dawa hizo kg 687.32 za skanga na kg1 ya hashishi zimekamatwa eneo la GOba, zikiw zimefichwa ndani y nyumba ya mtuhumiwa, uchunguzi umebaini kuwa wateja wengi wa skanka ni wananwake ambao hudai kutumia dawa hiz kunapunguza msongo wa mawazo na kujistarehesha", Aretas Lyimo Kamishna Jenerali DCEA.

Aidha mamlaka imefanikiwa kuwakamata vigogo wawili  wa madawa ya kulevya mkoani Dodoma.
"Mamlaka imewakamata watuhumiwa wawili Suleiman Mbaruku anayefahamika kwa jina la Nyanda(52), pamoja na Kimwaga Msobi(37), wakazi wa mtaa wa Kinyali kata ya viwandani wakiwa na kg 393 za heroin", Aretas Lyimo, Kamishna Jenerali DCEA.

Baadhi ya wananchi wanatoa maoni yao kwa Serikali namna wanayoweza kudhibiti biashara hiyo.
"Kwanza Elimu itolewe kwa wingi kuhusu madhara ya Dawa hizi hii inaweza kupunguza matumizi, matumizi yakipungua wauaji watakosa wateja kwahiyo wataachana na biashara hiyo", Jastina Kiambile, Mkazi wa Dar es Salaam.

"Nashauri wadili na wale vigogo wa juu kwa maana wakikamata hawa wa chini wao hawana ubavu wa kuingiza madawa haya kwahiyo wapambane kwanza na wale wanaoingiza dawa hizi", Gabriel Lucas, Mkazi wa Dar es Salaam

"Doria zifanyike huku mitaani maana dawa zinauzwa kama biashara nyingine hii itasaidia kupunguiza biashara hii",  Marco Samwel, Mkazi wa Dar es Salaam.

Aidha kupitia operesheni za kanda mamlaka hii imefanikiwa kukamata kilogramu 303 za bangi, gramu 103 za heroni pamoja na kilogramu 63 za mirungi katika maeneoe mbalimbali nchini.