Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi.
Kwa Mujibu kamanda wa Jeshi la Polsi Mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi amesema Mwamwere alikuwa anamfukuza mtoto huyo na alikimbilia kwenye jengo lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo bado lipo kwenye ujenzi na alipofika kwenye jengo hilo alimuua mjomba wake huyo kwa kumpiga kichwani kwa sululu na kutenganisha kichwa na kiwiliwili
Kamanda Msangi amesema Kufuatia tukio hilo mafundi waliokuwa wakiendelea na ujenzi walipiga kelele za kuomba msaada, hivyo kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi walijitokeza na kumshambulia mtuhumiwa kwa kumpiga hadi kufa na kisha kuuchoma moto mwili wake.
Marehemu wote walikuwa ni ndugu wanaoishi nyumba moja, miili yao imehifadhiwa hospitali ya rufaa mbeya na chanzo cha tukio hili kinachunguzwa ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu Yona alikuwa na matatizo ya akili.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 16.03.2015 majira ya saa 11:00 asubuhi huko katika mtaa wa nsalaga-uyole, kata ya nsalaga, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa pole kwa familia ya marehemu kutokana na tukio hilo. aidha anatoa wito kwa jamii/wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha katika mamlaka husika watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali kwa hatua zaidi za kisheria.