Simba SC inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama 22 itaweza kupanda mpaka nafasi ya pili msimamo wa ligi ikifanikiwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya KMC FC siku ya Jumatano Novemba 6.
Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ambapo mchezo wa Ligi Kuu namba 82 kati ya Simba dhidi ya KMC sasa utapigwa Jumatano, Novemba 6. Mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Jumanne ya Novemba 5 katika Uwanja wa KMC.
Mabadiliko mengine yaliyofanyika yanahusu mchezo wa Simba namba 89 dhidi ya Pamba Jiji ambao ulipangwa upigwe Novemba 21 sasa utapangiwa tarehe nyingine. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya ligi ya Tanzania kupitia kwa Msemaji wake Bwana Karim Boimanda.
Michezo ya ligi kuu itaendelea leo Novemba kwa michezo kuchezwa viwanja tofauti, kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Stadium Tabora timu ya Tabora United itakuwa Wenyeji wa Mashujaa kutoka Kigoma.Tabora United inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Pamba kutoka Mwanza.
Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera utachezwa mchezo utakaozikutanisha timu za Kagera Sugar dhidi ya Dodoma Jiji kutokea Dodoma.
Timu ya Yanga SC inaongoza msimamo wa ligi ya TPL licha ya kupoteza mchezo siku ya Jumamosi Oktoba 2 2024 dhidi ya Azam kwa kufungwa goli 1-0 goli lililofungwa na Gibril Sillah.Timu ya Wananchi imekusanya alama 24 kwenye michezo 9 ya ligi msimu huu. Singida Black Stars imesalia nafasi ya pili ikiwa na alama 23 baada ya kutoka suluhu ya kutokufungana na Coastal Union kutoka Tanga.
Simba SC inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama 22 itaweza kupanda mpaka nafasi ya pili msimamo wa ligi ikifanikiwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya KMC FC siku ya Jumatano Novemba 6.
Ligi kuu Tanzania bara msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa na ushindani huu unatarajiwa mpaka mwishoni mwa ligi kutokana na vikosi kuimarika baada ya kufanya mabadiliko ya mabenchi yao ya ufundi pamoja na kusajili vizuri katika dirisha kubwa la usajili la mwezi Julai 2024.