Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 majina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo yamekosekana kwenye orodha ya tuzo hizo. Zaidi ya miaka kumi na tano tuzo hizo zilitawaliwa na Wachezaji ambao wanatajwa kama Wachezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea Duniani Messi na Ronaldo.
Nyota wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Hispania Rodrigo Hernández Cascante, maarufu kama Rodri ameshinda tuzo ya Ballon D'or kwenye sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika Jiji la Paris nchini Ufaransa. Rodri ameshinda tuzo hiyo mbele ya Vinicius Junior wa Real Madrid aliyeshika nafasi ya pili, Jude Bellingham (Real Madrid) nafasi ya tatu na Dani Carvajal (Real Madrid ) ameshika nafasi ya nne.
Rodri alikuwa na msimu mzuri wa 2023-2024 alicheza michezo zaidi ya 50 mashindano yote ndani ya klabu yake pamoja na kushinda mataji ya ligi kuu Uingereza EPL, kombe la Klabu Bingwa Dunia, UEFA Super Cup na alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya UEFA EURO 2024 alipata majeraha katika mchezo wa fainali dhidi ya timu ya England.
Kiungo huyo wa The Citizens amejitengenezea sifa ya kuwa mmoja kati ya Wachezaji muhimu kikosi kinachonolewa na Pep Josep Guardiola, takwimu ya michezo ambayo City imecheza kiungo huyo akiwepo kikosini inaonyesha inawastani mzuri wa kushinda mihezo yake kuliko akikosekana. Yeye ndiye moyo wa timu hiyo yenye masikani yake Jijini Manchester na taifa la Hispania.
Wadau wengi wa Soka Dauniani waliamini Vinicius Junior ananafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo kulingana na kura zilizopigwa Muhispania Rodri ndiye aliyeibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2024.
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 majina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo yamekosekana kwenye orodha ya tuzo hizo. Zaidi ya miaka kumi na tano tuzo hizo zilitawaliwa na Wachezaji ambao wanatajwa kama Wachezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea Duniani Messi na Ronaldo.
Lamine Yamal wa Barcelona ameshinda tuzo ya Kopa Trophy tuzo ya Mchezaji bora wa Dunia kwa Wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 21 akifata nyota wengine wa klabu hiyo walioshinda kabla yake Pedri na Gavi.
Carlo Ancelotti ameshinda tuzo ya Kocha bora wa mwaka kutokana na mafaniko yake yakuiongoza Real Madrid kushinda ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Aitana Bonmatí anayecheza nafasi ya kiungo kwenye timu ya Wanawake ya Barcelona ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka 2024 kwa upande wa Wanawake.
Emiliano Martinez wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina amefanikiwa kutetea tuzo yake ya Golikipa bora wa mwaka baada ya kushinda tena tuzo hiyo jana usiku nchini Ufaransa. Martinez ameiongoza klabu yake kumaliza nafasi ya nne kwenye EPL pamoja na kushinda ubingwa wa kombe la mataifa ya America ya kusini.
Real Madrid imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kutokana na mafanikio yake kwenye mashindano ya klabu Bingwa barani Ulaya, hakuna Muwakilishi kutoka timu ya Los Brancos aliyehudhuria sherehe za usiku wa tuzo za 2024 Ballon d'Or usiku wa jana Paris Ufaransa ikiwa ni ishara ya kumsapoti nyota wao Vinicius Junior aliyekosa tuzo huyo wakidai yeye ndiye aliyestahili kushinda zaidi kuliko Rodri ambaye ameibuka mshindi wa tuzo hiyo.