Alhamisi , 24th Oct , 2024

Arne Slot atakiongoza kikosi chake cha Liverpool kukabiliana na Arsenal ya Mikael Arteta kwenye uwanja wa Emirates siku ya Jumapili Oktoba 27 mchezo utakaochezwa saa 9:30 Usiku kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu nchini Uiangereza.

Kocha wa Liverpool ya Uingereza Arne Slot raia wa Uholanzi  ameweka rekodi  ya Kuwa  Mkufunzi  wa kwanza kushinda michezo 11 kati ya 12 iliyocheza mwanzoni mwa msimu  na kuweke rekodi ya klabu hiyo

Kocha wa Liverpool ya Uingereza Arne Slot raia wa Uholanzi  ameweka rekodi  ya Kuwa  Mkufunzi  wa kwanza kushinda michezo 11 kati ya 12 iliyocheza mwanzoni mwa msimu  na kuweke rekodi ya klabu hiyo .

Hakuna Kocha aliyewahi kushinda michezo 11 kati ya 12 ya mwanzoni mwa msimu katika klabu hiyo yenye masikani yake katika Jiji la Anfield, Makocha wenye majina makubwa wameshapita kwenye klabu hiyo ya Majogoo ya Jiji lakini hawakufanikiwa kupata idadi kubwa ya ushindi kwenye michezo 15 ya mwanzoni ya klabu hiyo kama alivyofanya Slot.

Liverpool imeshinda goli 1-0 ugenini nchini Ujerumani kwenye mchezo wa ligi ya Mbingwa barani Ulaya dhidi ya Rasenball Sports Leipzig goli limefungwa na Darwin Nunez dakika ya 27 ya mchezo. Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha alama 9 baada ya kucheza michezo 3 ya mashindano ya Ulaya msimu huu.

Mabingwa mara 19 wa ligi kuu nchini Uingereza imeimarika kwa kiasi kikubwa chini ya Muholanzi huyo, inaongoza kwenye msimamo wa ligi nchini Uingereza ikiwa na alama 21, ikifuatiwa na Manchester City yenye alama 20 Vijana wa Mikael Arteta inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 17.

Wadau wa Soka Duniani walitegemea Kocha huyo wa zamani wa Feyenoord angepata wakati mgumu kwenye kibarua chake kipya kutokana na mafanikio ya Kocha aliyepita kabla yake Jurgen Klopp. Amewashangaza Mashabiki wa  timu hiyo ya Merseside kutokana na aina ya mpira inaoucheza timu ya  Liverpool.

Arne Slot atakiongoza kikosi chake kukabiliana na Arsenal ya Mikael Arteta kwenye uwanja wa Emirates siku ya Jumapili Oktoba 27 mchezo utakaochezwa saa 9:30 Usiku kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu nchini Uingereza.