Jumatatu , 21st Oct , 2024

Mamlaka zinazohusika na masuala mazima ya usalama wa barabarani nchini Marekani, (NHTSA) imeanza uchunguzi dhidi ya kampuni maarufu ya kutengeneza magari nchini huko inayofahamika kama Tesla.

 

Tesla ni moja kati ya makampuni yanayomilikiwa na Bilionea Elon Musk huku ikiwa ibeba sifa kubwa ya kutengeneza magari ya umeme ambayo kwa misingi ya utunzaji wa mazingira ni moja kati ya magari ambayo yanapendekezwa na mamlaka nyingi Duniani

ukiachilia mbali misingi ya kulinda mazingira na unafuu kwenye matuzo na uendeshaji wa gari hilo, moja kati ya kesi kubwa kwa sasa ni mamlaka ya usalama ya nchini Marekani kuwa na hofu na mfumo uliletwa na kampuni hiyo unaofahamika kama ''Full Self Driving'' kwa maana fupi ukiiingia kwenye gari hii wewe ni kukaa na kuweka uelekeo tu mengine yote utaiachia akili mnemba itafanya sehemu yake.

Mmalaka hiyo inayohusika na usalama wa Barabarani imesema kwa sasa inafanya uchunguzi kuhusu mfumo huo wa ''Full Self Driving'' na hii ni mara baada ya uwepo wa kesi 4 za ajali na moja ikiwa ni ya kumgonga mtembea kwa miguu.

Mamlaka hiyo imesema inafanya utafiti kufahamu, kwamba iwapo mfumo huo unaweza kutambua barabara za aina tofauti na pia hali za hewa kama vile jua kali, ukungu na mvua kubwa  na vile vile kutamani kufahamu iwapo kumewahi kutokea ajali nyingine zilizosababishwa na mfumo huo na hazikutolewa taarifa.

Nb: NHTSA ni kifupi cha The National Highway Traffic Safety Administration’s