Harris mwenye umri wa miaka 59, anagombea dhidi ya Trump mwenye umri wa miaka 78, katika ikulu ya White House mwezi Novemba.
Katika kinyang'anyiro hicho kikali, timu ya kampeni ya Harris ina matumaini kwamba kulinganisha ujana wake na uwezo wa kiakili na umri wa juu zaidi wa , itasaidia kuwashawishi wapiga kura wasio na uamuzi kwamba anafaa zaidi kwa ofisi kuliko yeye.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alihoji afya ya rais Joe Biden wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 81 alipokuwa anataka kuchaguliwa tena. Tangu Biden alipobadilishwa kwa tiketi na Harris, afya ya Trump mwenyewe imevutia zaidi.
Kwa mujibu wa msaidizi wa Harris, makamu huyo wa rais alitoa taarifa zake za kimatibabu kwa umma siku ya Jumamosi katika juhudi za kuangazia hatua ya Trump kukataa kufanya hivyo.
Trump ametoa taarifa chache sana za kiafya, ikiwemo baada ya sikio lake kugongwa na risasi wakati wa jaribio la mauaji mwezi Julai.