Mwili huo umeguduliwa kuwa ni wa mwanamke aitwae Arnota Luchende (53 ) ambaye mara ya mwisho alionekana tarehe 6 mwezi huu kabla ya kupotea .
Kaka wa marehemu amesema kuwa dada yake aliondoka nyumbani jumanosi 5 Okbota 2024 lakini hakuwahi kurejea nyumbani.
Taarifa zinasema kuwa matuko ya kutupwa miili ya watu waliouawa yanarindima katika eneo hilo.
Agosti 22, mwaka huu, wakazi wa eneo la Isango mpakani mwa maeneo bunge ya Navakholo na Lurambi, waliamka kwa mshtuko mkubwa baada ya kukuta miili miwili ya wanawake wasiojulikana ikiuawa kwa namna hiyo.
Wanawake hao wawili walionekana kuwa wamenyongwa na ndimi zao zilikuwa hazipo . Miili yao pia ilikuwa imefungwa katika magunia meupe na kuzusha hofu kwamba vifo hivyo vilikuwa vya imani za kishirikina.
Septemba 19, karibu na eneo la Shirakalu, mwili wa mwanamke mwingine ulikutwa umetupwa kando ya barabara na karibu na eneo hilo kulikuwa na gunia jeupe.