Jumatatu , 5th Mei , 2014

Klabu ya Yanga imesema kuwa haina tatizo na kuondoka kwa wachezaji wake Frank Domayo na Didier Kavumbagu na kuwataka wanachama wake wawe watulivu kwa kuwa wachezaji hao wanatafuta maisha.

Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu (kulia) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga

Uongozi wa makamu bingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Dar Young Africans umesema kukaa kwao kimya katika kipindi hiki ambacho wanachama wa timu hiyo wamekua wakiutupia lawama uongozi huo kwa kuwaachia wachezaji nyota wawili wa timu hiyo kujiunga na Azam FC si kwamba shughuli za kiutendaji katika majukumu ya klabu hiyo hazifanyiki.

katibu mkuu wa klabu hiyo Beno Njovu amesema wao kama viongozi wanaendelea na majukumu yao kama kawaida na kitendo cha wachezaji hao kuondoka ni cha kawaida kwani nao wanatafuta maisha, na wao kama kamati ya utendaji wanaendelea na shughuli ya usajili kimya kimya kwa kushirikiana na benchi la ufundi.