Alhamisi , 1st Mei , 2014

Shirikisho la soka Tanzania TFF linaanza kufanya uchunguzi juu ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya klabu za soka kuwasajili wachezaji ambao wako katika kambi ya timu ya Taifa kinyume na utaratibu.

Frank Domayo akisaini mkataba na klabu ya Azam

Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.

Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.

TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.