Jumatano , 9th Oct , 2024

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda amewaonya watumishi na watendaji wa serikali mkoani arusha wanaokwamisha wafanya biashara kwa maslahi binafsi na wale wanao walipisha wafanya biashara ili wapate upendeleo au nafasi (network) ya kuonana na kiongozi wa serikali.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishina watendaji wa serikali ofisini kwakwe ambapo amesema hatosita kuwachukulia hatua na endapo atakapo bainika mtu anaefanya hivyo kibarua chake kitakuwa kimeishia hapo.

“Nisingependa kusikia ya kwamba kuna mfanya biashara anaonewa au anatishwa atoe fedha ili apate network, au jambo lake linakwamishwa ilia toe fedha. naomba tuelewane mtendaji atakae bainika kwenye ngazi yeyote ile anamkandamiza mfanya bishara ili achukue pesa kibarua chake kitakuwa kimekoma hapo hapo.” Ameseama Paul Makonda