Jumanne , 8th Oct , 2024

Ukosefu wa elimu na kutokupata matibabu sahihi mara kwa mara imeelezwa kuchangia katika uoni hafifu wa ghafla kwa jamii nahivyo kupelekea utendaji kazi usio na ufanisi

Daktari bingwa wa kliniki ya Macho ya Majey Smart Version Jafar Majala akieleza jinsi ukosefu wa elimu na tabia ya kutokupima macho mara kwa mara imechangia katika kupata matatizo ya ghafla ya uoni

Katika Kupambana na magonjwa ya uoni  daktari bingwa wa macho Jafar Majala ameeleza kuwa ukosefu wa elimu na tabia yakutokupima macho mara kwa mara imechangia katika kupata matatizo ya ghafla ya uoni hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

"Tunaposema afya ya macho tunamaanisha kwamba uoni wa kawaida kwa mtu yeyote kwa rika zote, kunawatu wanamatatizo mbalimbali ya macho ambayo either kwakujua au kwakutokujua hawapatiwi matibabu sahihi. Kwahiyo nivyema kila mwanajamii akajitengea utaratibu wakupima macho atleast maramoja kwa mwaka". Amesema Jafar Majala, Daktari bingwa wa Macho Majey Smart Version- Kliniki ya Macho

Aidha baadhi ya wananchi wameongeza kuwa wengiwao hawana mazoea yakwenda kupima mara kwa mara hivyo kupelekea kuumwa macho kwa kushitukiza bila kujua.
"mwanzo nilikuwa sijui kwamba kulikua na magonjwa niyakurithi yanasababisha upofu wa macho kwahiyo ni vyema mtu au kijana kupima mara kwa mara macho". Amesema Duke Ibrahim, Mkazi wa vingunguti,  Dar es salaam
"watu wengi wanaumwa ugonjwa wa macho maranyingi kutokana na kutopima mara kwa mara ushauri nikwenda kupima mara kwa mara ilitujue tatizo la macho". Amesema Adam Uota Chota - Mkazi wa Msasani, Dar-es-Salaam 

Nae kwa upande wake John Elisha mkazi wa kinondoni ameeleza ukosefu wa elimu kutolewa kwa wananchi imechangia wengi kukosa uelewa wa madhara na namna yakupata huduma yakupima macho.

"kwanza watu hatuna elimu yakupima afya mara kwa mara na mtu huwa ni mpaka changamoto impate ndipo aende hospitali kupima kwahiyo ninachoshauri elimu itolewe huku watu washauriwe  ili tudhibiti tatizo kabla halijamkuta". John Elisha amesema.

Siku ya Afya ya Macho Duniani huadhimishwa tarehe 10 Oktoba kila mwaka. Siku hii inalenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa afya ya macho na kukuza hatua za kuzuia na kutibu magonjwa ya macho.