Jumatatu , 7th Oct , 2024

Mshambuliaji wa Barcelona raia wa Polandi Robert Lewandoski alifunga hat-trik ugenini dhidi ya Deportivo Alaves na kuiwezesha Barcelona kuongoza La Liga kwa tofauti ya pointi 3 mbele ya kikosi cha Real Madrid, Lewandoski amefunga goli 13 katika michezo 11 ya mashindano yote msimu huu

Robert Lewandoski alifunga hat-trik na kuipaisha Barcelona kileleni katika msimamo wa  La Liga kwa tofauti ya pointi tatu mbele ya Mahasimu wao wakubwa Real Madrid kutokana na ushindi walioupata  ugegeni dhidi ya Deportivo Alaves.

Ushindi wa Real Madrid siku ya Jumamosi katika dimba la Santiago Barnabeu dhidi ya Villareal uliwafanya kufikisha alama sawa na kikosi cha Hansi Flick kabla ya kucheza jana dhidi ya wapinzani wao wanaotoka jiji moja la Barcelona.

Miamba ya Catalunya ambayo ilipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Osasuna, walionekana wanahitaji ushindi kwa kiasi kikubwa walifunga mapema kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Polandi Lewandoski baada ya kupokea pasi kutoka Rafinha.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, alifunga goli lake la pili kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mbrazil aliye katika kiwago bora sana kiuchezaji tangu ujio wa kocha raia wa Ujerumani  ndani ya Barca.

Goli la tatu walilofunga Barcelona,  limetokana pasi ya   Eric Garcia kwa mshambuliaji wao hatari aliyewahi kuzitumikia  Borrusia Dortmund na Bayern Munich zote za nchini  Ujerumani  raia wa Polandi.

Lewandoski mpaka sasa ameshafunga goli 13 katika michezo 11 ya mashindano yote akiwa na jezi ya mabingwa wa La Liga msimu wa 2022-2023 wenye  wastani wa kufunga goli tatu au zaidi kwenye michezo ya ligi kuu nchini Hispania msimu huu.