Jumatatu , 30th Sep , 2024

Majeshi ya magereza nchini yametakiwa kutumia rasilimali zilizopo katika kufanya uzalishaji mkubwa kupitia kilimo kwani Serikali imewekeza miundombinu itakayowezesha kilimo kufanikiwa kwa urahisi.

Waziri masauni akisalimiana na maafisa wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai

Wito huo umetolewa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alipotembelea Maafisa wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai, Mbinga Mkoani Ruvuma na kuwataka kutumia rasilimali kuongeza uzalishaji.
"Haiwezekani miaka 55, mnalima less than 10%, katika mazingira ya sasa hivi ambayo serikali imiweka kipaumbele katika mambo ya kilimo, maji yanamwagika [pale mnatakiwa mfanye uzalishaji mkubwa wa mashamba", alisema Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa mambo ya ndani.

Aidha Masauni amewataka magereza kufanya mabadiliko ya  kimuundo na kitaasisi ambayo yatakwenda kuongeza uwezo wa uzalishaji mazao ya kilimo kwa magereza ya uzalishaji mali nchini. 
"Miongoni mwa maboresho hayo ni kutenganisha mamlaka ya kiutawala ya Jeshi la Magereza na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo (SHIMA), ambapo maboresho yatakwenda kuleta ufanisi wa usimamizi wa mauasala ya kiutawala na biashara", alisema Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa mambo ya ndani.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai SP. Gabriel Luderi amesema Gereza hilo lipo tayari kupokea na kuendana na mabadiliko yakatayoongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.
"Kama ulivyosema fursa sasa  hivi, mazingira yameboreshwa  sana tunaa ahidi kufanya mabadiliko ya kimiundo ili tuweze kuzalisha kwa tija na kuendana na kasi ya mabadiliko ya kimundo", alisema Sp. Gabriel Luderi, Mkuu wa Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai