Wakati mashabiki wa Yanga wakitambia kikosi chao kushinda kwa idadi kubwa ya mabao dhidi ya Ken Gold, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamond amesema anachotaka ni pointi tatu, lakini wapinzani wao wakijichanganya watawapiga nyingi.
"Denis Nkane kwangu namuona ana uwezo wa kuwa beki wa pembeni anayeweza kushambulia (wingback) kwasababu ana kasi na ujuzi, naamini hii nafasi itamjenga kuwa bora zaidi kwenye siku za usoni''Miguel Gamondi
Kocha huyo ameongeza ku
wa wachezaji wote walosafiri wako fiti isipokuwa wanamkosa Farid Mussa ambaye ni majeruhi, akieleza kuwa Yanga inao nyota wengi na wenye uwezo hivyo wanasubiri muda ufike waingie uwanjani.
Kuhusu ratiba yao na hali ya uchovu, Gamond amesema hana hofu yoyote kwani wachezaji wake wanao uzoefu na uwezo binafsi na anachoweza kufanya ni kufanya maboresho