(Mohamed Salah akishangilia moja la bao lake ndani Liverpool)
Salah mwenye umri wa miaka 32 bado hajasaini kandarasi mpya ndani ya Liverpool huku alisaini mkataba mpya wa miaka 3 mnamo Julai 2022 huku akiweka rekodi ya mchezaji anayelipwa fedha nyingi ndani ya Anfield kiasi cha Pauni 350,000 kwa wiki sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 kwa fedha za Kitanzania.
Liverpool ilikataa ofa ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia kwa dau la Pauni Milioni 150 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 537.2 kwa fedha za Kitanzania huku nahodha huyo wa Misri alijiunga na Liverpool akitokea klabu ya AS Roma kwa dau la Pauni Milioni 34 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 121.8 mnamo mwaka 2017 huku mpaka sasa amefunga magoli 213 kwenye michezo 351 na kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya Liverpool akishika nafasi ya 5.