Alhamisi , 29th Aug , 2024

Timu ya Southampton imefikia makubaliano ya awali na Arsenal kumsajili Golikipa Aaron Ramsdale kwa dau la Pauni Milioni 25 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 89.4 kwa fedha za Kitanzania huku usajili huo ukitaraji kukamilika kabla ya dirisha la usajili halijafungwa Ijumaa ya Agosti 30-2024

(Aaron Ramsdale akiwa kwenye majukumu yake ndani Arsenal FC)

Mwingereza Ramsdale mwenye umri wa miaka  26,Amekuwa chaguo la pili ndani ya Arsenal mbele ya Mhispania David Raya aliyejiunga akitokea kwa mkopo ndani ya timu ya Brentford msimu 2023-24 na kumfanya Ramsdale kucheza michezo 6 pekee ndani ya msimu uliopita ndani ya Arsenal.

Aaron Ramsdale aliitumikia Arsenal kwenye michezo yote ya Epl msimu 2022-23 waliomaliza nafasi ya pili nyuma ya Manchester City huku ameitumikia timu ya England kwenye michezo 5 huku mchezo wa mwisho alicheza dhidi ya Iceland kwenye mchezo wa mwisho kabla ya shindano la EURO 2024 nchini Ujerumani.