Jumanne , 27th Aug , 2024

Nyota Mserbia Novak Djokovic ameanza kwa ushindi kwenye michuano ya wazi ya tenisi ya Marekani (US Open) kwa ushindi wa seti tatu mfululizo 6-2 6-2 na 6-4 dhidi ya Radu Albot kutoka Moldova kwenye mchezo wa raundi ya kwanza wa michuano hiyo uliochezwa leo Agosti 27-2024 nchini Marekani

(Nyota wa Tenisi Mserbia Novak Djokovic)

Djokovic mwenye umri wa miaka 37 amesema "ushindi huu ni kisasi dhidi ya ndugu zangu Djordje na Marko waliopoteza mbele ya wachezaji wa Moldova  akiwamo na Albot siku za nyuma japo huu ni utani tu kwangu binafsi".

Novak Djokovic anayeshikilia mataji 24 ya Grand Slam sawa na Mwanamama Margaret Court huku akiwa anasaka taji la 25 kwenye shindano la US Open 2024 huku sasa atapambana na Mserbia mwenzake Laslo Djere kwenye mzunguko wa pili mnamo Jumatano ya Agosti 27-2024