Alhamisi , 25th Jul , 2024

Usiku wa jumanne wiki hii, Huko Italia kwenye mji wa Milan kulishuhudiwa tetemeko la Ardhi kwa sekunde kadhaa, na si kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi la hasha! ni kwa sababu ya mwanamuziki wa kuitwa Travis Scott 

 

Kwenye ziara yake aliyoipa jina la Utopia ikiwa kama jina la album yake iliyotoka July 28, 2023 ilishika sura mpya baada ya kufika kwenye jiji la Milan na kuhudhuriwa na idadi ya watu ambayo iliwashangaza waliowengi ulimwenguni kote,

Ziara hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu zaidi ya ''80,000'' ni sawa na kusema uwanja mzima wa Real Madrid unaofahamika kama  Santiago Bernabéu ambao unapokea idadi hiyo ya watu.

Mtangazaji wa kipindi cha The Cruise kutoka EastAfricaRadio Connie Beily anasema kilichofanywa na Travis ni hitsoria kwenye muziki wa mtu mweusi ulimwenguni na Travis kwa mara ya kwanza amevunja rekodi iliyowekwa na Drake kwenye ziara yake pale Washington, D.C kwa kujaza mashabiki zaidi ya elfu thelathini na nne ''34,000''