Mtanda ametoa wito huo leo tarehe 22 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa wadau wa maendeleo ya mpira wa miguu uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana ulioenda sambamba na uzinduzi wa uuzwaji wa tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo.
Amesema ni wakati sasa kwa watu wote wenye maoni ya kuboresha timu hiyo kwenda kwenye uongozi wa timu hiyo kufanya hivyo na sio matamanio ya watu wachache kwa timu za nje ya Mkoa huo kusababisha siku za mechi kwenye msimu ujao wakajitokeza watu kuwapokea wageni.
"Tumedhamiria kurejesha furaha za wanapamba kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi ambayo wameikosa kwa zaidi ya miaka 23, tunawashukuru sana wachezaji wetu wa zamani waliopo na waliotangulia mbele za haki". Mhe. Mtanda.
Aidha, amewataka mashabiki wa timu ya Pamba Jiji kuipa uhshirikiano wa kutosha timu yao kwani imekamilika kutokana na usajili mzuri uliofanywa kwenye mchujo wa zaidi ya wachezaji 900 na akabainisha kuwa pamoja na usajili wa wachezaji kutoka nje wapo wachezaji wazawa kwenye kikosi hicho maarufu kama TP Lindanda.
Tamasha la siku ya Pamba linatarajiwa kufanyika agosti 10, 2024 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na wasanii mbalimbali watokanao na Mkoa wa Mwanza watatumbuiza wakiongozwa na Fid Q pamoja na wakubwa wa nje ya Mkoa wakiongozwa na Harmonize (Konde boy).