Kocha wa Simba SC Fadlu Davids
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam,Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amesema mkufunzi mkuu wa klabu hiyo Fadlu Davids amelizishwa na kikosi cha Simba kutokana na umri unaofundishika,wana nguvu na morali na anaimani kikosi hicho kitafanya mazuri kwa ajili ya msimu unaokuja 2024-25.
Simba SC imeweka kambi ya wiki tatu mjini Ismailia nchini Misri huku kikosi hicho kinaraji kurejea nchini mwanzoni mwa mwezi Agosti kwa ajili ya kujiandaa na tamasha la Simba Day litakalofanyika mnamo Agosti 03-2024 Jijini Dar es Salaam.