Alhamisi , 27th Jun , 2024

Aliyekuwa mshambuliaji wa FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mtanzania George Mpole, amesema bado hajasini timu yoyote licha ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Baada ya taarifa nyingi kuwa mshambuliaji huyo amemalizana na uongozi wa Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2024/25 wa mashindano,

EATV  ilimtafuta Mpole ambaye amesema tayari amepokea ofa nyingi ndani ya nchi ikiwemo Yanga na timu nyingine lakini pia kutoka nje ya nchi.
-
“Ni mchezaji huru baada ya mkataba wangu na Lupopo kufikia tamati. Ofa zipo nyingi siwezi kuzitaja zote hizo. Yanga na Simba nipo nao kwenye mazungumzo na kikubwa naangalia kwenye ofa ambayo nimeitaka,” amesema Mpole.

-
Ameongeza kuwa bado hajaafikiana na klabu yoyote kati ya hizo kwa sababu mazungumzo yanaendelea,yeye anaangalia maslahi pamoja na nafasi ya kwenda kucheza.
-
Mpole aliwahi kuwa mfungaji bora wa msimu wa 2020/21 wa Ligi Kuu Bara akiwa na jumla ya mabao 17 na pasi 4 za mabao wakati anacheza Geita Gold FC ambayo imeshuka daraja, huku akifuatiwa na mshambuliji wa Yanga, Fiston Mayele aliyemaliza msimu akiwa na mabao 16 na pasi 5 za mabao.