Jumapili , 19th Mei , 2024

China imesema itaendelea kufadhili miradi mipya ya kimkakati ya Tanzania inayoendelea, baada ya kuridhishwa na utekelezwaji ya miradi ya awali. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Misaada la China (CIDCA), Luo Zhaohui, ameyasema hayo kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, yaliyofanyika jijini Beijing, China.

Zhaohui amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaweza kusaini mikataba mipya ya ushirikiano na misaada Septemba mwaka huu pembezoni mwa mkutano wa Wakuu wa Nchini na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) ambao amealikwa tayari.

CIDCA ndiyo taasisi inayopitisha misaada na mikopo ambayo serikali ya China kutoa kwa nchi zote duniani na Waziri Makamba alikwenda kufanya mazungumzo na mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayoendelea nchini China.