Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.
Kwa mujibu wa Babu wa kijana huyo anayefahamika kwa jina Benson Masuni, amesema mjukuu wake alilazwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na kesho yake baada ya kutoka alifika nyumbani na kujitundika kwenye mti wa muembe muda ambao hakukuwa na mtu nyumbani hapo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo ambalo chanzo chake kinatajwa huenda ni msongo wa mawazo uliotokana na kuugua muda mrefu.