Mtoto aliyeunguzwa mikono kwa maji ya moto na mama ambaye ni jirani yake
Wazazi wa mtoto huyo wamesema mtuhumiwa alikamatwa hata hivo tayari amepewa dhamana, hivyo kuomba serikali ichukue hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Majengo mapya Raphael Mathias amekemea kitendo hicho na kuwataka wananchi waache kujichukulia sheria mkononi.
Huu ni mwendelezo wa matukio kadhaa ya ukatili dhidi ya watoto Jijini Mwanza ambayo yameripotiwa na EATV hivi karibuni.