Jumanne , 5th Mar , 2024

Katika hali isiyo ya kawaida  wananchi wa kijiji cha Iwungilo  wameshindwa kuzuia hisia zao mbele  ya mkutano  wa hadhara wa kusomewa  mapato na Matumizi ya Kijiji Baada ya mwenyeki wa  Kijiji hicho Joseph Myamba kutangaza kuachia nafasi hiyo  baada ya  kuwasomea mapato na  matumizi

Awali akifungua Mkutano Mwenyekiti  huyo ameanza kwa kuwataka wananchi kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo ili waweze kufikia malengo yao ya  mafanikio  na hatimaye  anatamka kauli inayo washitua wananchi ya kutaka kujiuzulu nafasi hiyo.

Licha ya mwenyekiti wa kijiji hicho kusita kueleza chanzo cha cha kutaka kujihuzulu nafasi hiyo  wananchi wa kijiji katika mkutano huo  wakasema hakuna haja ya kuficha ukweli kwani wao wanajua  chanzo cha kiongozi  wao huyo kutaka kuachia ngazi ni  kuenguliwa kwenye kamati ya   ujenzi wa kituo cha afya  cha kata  unao endelea kutekelezwa kijiji hapo.

Kutokana na hali hiyo kituo hiki kimelazimika kumtafuta diwani wa kata ya Iwungilo ili kujua ukweli juu ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa kijiji cha Iwungilo kwenye kamati  hiyo kama wananchi walivyoeleza katika mkutano.