Msanii Juma Mohamed Mchopanga maarufu kama Jay Moe.
Jay Moe ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio Jijini Dar es salaam.
Hii inasaidia hata ukiangalia wasanii wa mbele kama kina Amber Rose au Kim Kardashian ila wenyewe wanafanya hivyo wakiwa na malengo maalumu kulingana na mashabiki wanavyowachukulia.
''Mfano mimi siwezi tengeneza kiki eti Jay Moe anatoka na mtu fulani kwa sababu kwanza aina ya muziki wangu na mashabiki wangu siyo wa aina hiyo ila kwa mtu anayeimba mapenzi anaweza fanya hivyo kwa kuwa mashabiki wake wengi ni kinadada ambao wanapenda kufuatilia mambo kama hayo.
Hata hivyo Jay Moe amesema pamoja na kufanya hivyo ni lazima msanii awe amejipanga vizuri kwenye mitandao ya kijamii kwani ndiyo inaweza kusaidia hizo skendo.
Jay Moe anakubalika sana kwa kazi zake na baadhi ya ngoma zake ni kama Bishoo,Jua na mvua,Kama unataka demu, Maisha ya boding, Stori tatu tofauti.

