Klabu ya soka ya Ihefu yenye Makazi Yake Jijini Mbeya imejikuta ikipitia katika kipindi kigumu baada ya kucheza zaidi ya mechi 7 pasi kuambulia ladha ya Ushindi
Ihefu hii Leo imeshinda 3-2 ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar huku mabao Yao yakifungwa na wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la mwezi January kutokea Singida Fountain Gate FC
Mabao mawili ya Ihefu yaliwekwa kimiani kipindi cha kwanza na Marouf Tchakei na Duke Abuya wakati lile la ushindi lilifungwa kipindi cha pil cha mchezo na Elvis Rupiah