Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na nyota Frank Kessie na Sebastian Haller huku bao la Nigeria likifungwa na mlinzi Troost Ekong huku Super Eagles ambao ni washindi wa pili wameondoka na Dola Milioni 4 (4,000,000) zaidi ya Bilioni 10.1 kwa fedha za Kitanzania
Upande mwingine, Golikipa Ronwen Williams wa Afrika Kusini ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano,Emilio Nsue Lopez ameshinda tuzo ya mfungaji bora baada ya kuifungia Equatorial Guinea mabao5 ilhali nahodha wa Nigeria William Troost-Ekong akichaguliwa kuwa mchezaji bora mashindano ya Afcon 2023.