Jumamosi , 16th Dec , 2023

Mtoto wa miezi minne amepatikana akiwa hai "kwa neema ya Mungu" wazazi wake walisema baada ya mtoto huyo kunusurika  katika kimbunga huko Tennessee.Wanandoa hao walisema kimbunga kikali siku ya Jumamosi kiliharibu nyumba yao .

Alinusurika na kugunduliwa katika mti ulioanguka wakati wa mvua ya kubwa. Mtoto huyo, kaka yake wa mwaka mmoja na wazazi wake walipatwa na majeraha kutokana na kukatwa na miti iliyowasababishia michubuko midogo.

Wakati kimbunga hicho kikikaribia, mama wa watoto wawili, Sydney Moore, mwenye umri wa miaka 22, alisema paa la nyumba yao  lilikatwa.

"Ncha ya kimbunga ilishuka na kuchukua bassinet na mtoto wangu, Bwana, ndani yake," Bi Moore aliiambia kituo cha habari cha eneo hilo.