
Sasa taarifa mpya kutoka google ni kuhusu kuzifuta G-Mail account, ambazo zimechukua zaidi ya miaka miwili bila ya wamiliki wake kuzitumia. (inactive accounts)
Kibaya zaidi kuhusu hizi G-Mail account ambazo zitafutwa kuanzia tarehe 1/12 zitafutwa na kila kilichomo ndani yake kwa maana ya picha, emails, videos, calendar event na kila kilichomo ndani yake.
Njia ambayo unaweza kuepukana na adha hii ikiwa kama una-G-mail account ambayo hujaitumia kwa zaidi ya miaka 2 hivi sasa, ni kuingia kwenye G-Mail account yako (log in) ili kujihakikishia usalama zaidi kwenye upande huu.
Picha: hipertextual.com