Jumanne , 24th Oct , 2023

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki amemzawadia mpira Waziri wa Madini Antony Mavunde baada ya mchezo dhidi ya Azam FC.

Azizi Ki amemzawadia Mavunde mpira aliopewa baada ya kufunga 'hat-trick' na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mavunde aliongozana na Rais wa Yanga Hersi Said kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na ndipo staa huyo Mbukinabe akampatia zawadi hiyo.

Aziz Ki anakuwa mchezaji wa tatu kufunga ‘hat-trick’ Ligi Kuu Bara 2023/2024 akiungana na Feisal Salum ambaye naye alifunga kwenye mchezo kati ya Azam na Tabora United na Jean Baleke wa Simba akiifunga Coastal Union.