Jumatano , 18th Oct , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Samia akiwa kwenye Soko la Nzega Parking

Rais Dkt. Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko hilo ambapo mbali na ujenzi wa soko lakini pia ametoa mitaji kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa soko hilo.

Aidha Rais Dkt. Samia amewataka wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.