![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/09/24/Snapinsta.app_378840726_18309583681110519_2432508498469451656_n_1080.jpg?itok=Skcwx6L_×tamp=1695558336)
Gari hiyo ambayo Che Malone alikuwa dereva iliingia mtaroni akiwa anamkwepa dereva pikipiki (Bodaboda), hata hivyo ni mtu mmoja tu ambaye ni kaka yake Che Malone aliyekuwa amekaa siti ya mbele ndiye aliyeumia kidogo na kupelekwa hospitali na baada ya matibabu akaruhusiwa kutoka.
Gari hiyo ilibeba watu wanne, akiwemo dereva Che Malone. Ukiachana na kaka yake Che Malone ambaye ndiye aliyeumia ,wengine wote hakuna aliyeumia kabisa.
Simba kupitia msemaji wake Ahmed Ally imethibitisha beki huyo yupo salama na kesho atakuwepo mazoezini na wenzake.