Jumatatu , 18th Sep , 2023

Mkacha Mohamed Mkacha (23) mkazi wa Soya, Chemba mkoani Dodoma, amepoteza maisha  kwa kuanguka na pikipiki, wakati akiwakimbia Askari Polisi wa Kibaya, Kiteto mkoani Manyara akiwa amepakia abiria na madawa ya kulevya aina ya mirungi bunda 250 sawa na kilo 119.

Pikipiki

Akizungumza na EastAfricaTV Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara ACP George Katabazi, ameeleza jinsi ilivyokuwa.

"Tulifanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 250 sawa na kilo 119 akiwana mwenzake  wakiwa na usafiri wa pilipiki iliyokuwa imeondolewa namba ili wasifahamike, tukio limetokea baada ya polisi kupata taarifa za kiintelejensia na walipogundua kuwa wanafuatiliwa walikimbia kwa spindi kali kisha walipata ajali na mtuhumiwa mmoja kufariki," amesema Kamanda Katabazi.

Hata hivyo Kamanda Katabazi ameeleza kuwa marehemu alifariki wakati akipatiwa matibabu hospitali ya wilaya ya Kiteto