
Habib Nsikonnene akiwa na wake zake
Nsikonnene anatajwa kuwa ndiye mwanaume tajiri mkubwa kijijini hapo ukilinganisha na vipato vya wenzake, hadi imepelekea mwenyekiti wa kijiji hicho kutaka kuipa moja ya barabara jina lake, kwani shughuli yake ya uganga inamuingizia pesa nyingi, na ni kama shujaa kijijini hapo kwani kimekuwa maarufu kwa sababu yake.
"Nsikonnene yupo kijijini hapa kwa takribani miaka minne, alikuja na kununua ardhi hapa na kujitambulisha kwangu kuwa yeye ni mganga wa kienyeji, tukamruhusu kufanya biashara yake, alipoishi hapa, hatukujua kwamba angetuletea umaarufu, jina la kijiji chetu linavuma kila mahali," amesema Emmanuel Owere, Mwenyekiti wa Kijiji cha Namasengere.