Jumamosi , 19th Aug , 2023

Jumuiya kuu ya Afrika Magharibi imekubaliana juu ya  uwezekano wa kuingilia kijeshi kurejesha demokrasia nchini Niger baada ya majenerali kumpindua na kumshikilia Rais Mohamed Bazoum mwezi uliopita.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imekubaliana Ijumaa (18.09.2019) kuanzisha kikosi cha kusimama kama njia ya mwisho ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa, afisa mwandamizi alisema bila ya kutoa maelezo ni lini.

"Tuko tayari kwenda wakati wowote amri itakapotolewa," Kamishna wa Masuala ya Siasa, Amani na Usalama wa ECOWAS Abdel-Fatau Musah alisema wakati wa sherehe za kufunga mkutano wa siku mbili wa wakuu wa majeshi ya Afrika Magharibi katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

"Siku ya D-Day (maamuzi) pia inaamuliwa. Tayari tumekubaliana na kuweka sawa kile kitakachohitajika kwa kuingilia kati," alisema, akisisitiza kuwa ECOWAS bado inataka kushirikiana kwa amani na viongozi wa kijeshi wa Niger.
Wakuu wa ulinzi walikutana na maelezo ya kina juu ya uwezekano wa operesheni ya kijeshi ya kurejesha Bazoum ikiwa mazungumzo yanayoendelea na viongozi wa mapinduzi yatashindwa.

"Tusiwe na shaka kwamba ikiwa kila kitu kingine kitashindwa, vikosi vya kishujaa vya Afrika Magharibi, jeshi na raia, viko tayari kuitikia wito wa wajibu," alisema Musah.

Maafisa wa jeshi walimng'oa madarakani Bazoum mnamo Julai 26 na wamekaidi wito kutoka kwa Umoja wa Mataifa, ECOWAS na wengine wa kumrudisha.