
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo
Katibu Mkuu Chongolo amesema hayo leo Ijumaa, Juni 16, 2023 alipokuwa akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma, ambayo iko siku ya pili, akiwa ameanzia wilaya ya Mpwapwa.
Akizungumzia baadhi ya maeneo mahsusi, akiwa Kibakwe wilayani Mpwapwa, amepongeza kwa namna ilivyojielekeza kulinda viwanda vya ndani, utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya vyuo vya elimu ya kati, pamoja na kuondoa zuio la kufunga biashara jambo ambalo lilikuwa linasababisha uadui kati ya taasisi za serikali na wananchi, hususani wafanyabiashara.
Kuhusu mikopo kwa vyuo vya elimu ya kati Chongolo amesema uamuzi huo umelenga kuandaa na kuzalisha wataalamu wengi kupitia vyuo vya kati.
Katika ziara hiyo ambayo imelenga kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kuhamasisha uhai wa CCM katika ngazi ya mashina/mabalozi na kukagua miradi ya maendeleo kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025, Chongolo ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa wa Oganaizesheni Ndg Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema.