Jumanne , 29th Jul , 2025

Ben-Gvir amewahi kudai kuwa Wapalestina wote wanahusika, alipokuwa akitetea kuzingirwa kwa ukanda huo.

Uholanzi imewapiga marufuku ya kutoingia katika taifa hilo (persona non grata) mawaziri wa Israel wenye msimamo mkali, Bezalel Smotrich na Itamar Ben-Gvir kutokana na matamshi yao ya “usafishaji  wa kikabila”huko Gaza, Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi amesema  viongozi hao wawili wamekuwa ni wachochezi wa vurugu za mara kwa mara, na pia wameunga mkono makazi ya kiyahudi yasiyo halali na kitendo cha kutaka Gaza ivamiwe tena.

Ben-Gvir amewahi kudai kuwa Wapalestina wote wanahusika, alipokuwa akitetea kuzingirwa kwa ukanda huo.

Uholanzi imesema kuwa huenda ikaunga mkono vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Israel ikiwemo kusitisha ushirikiano wa utafiti,endapo Israel itaendelea kuzuia misada kwenda Gaza.