Mtangazaji TBway 360 na mpenzi wake Kim Nana
Akikata mzizi wa fitna wakati anazungumzia suala hilo kupitia EATV & EA Radio Digital T Bway ameeleza kuwa
"Sidhani kama nikawa nipo na mtoto halafu mama yake asiwepo au mpaka tupige picha ndiyo mjue kwamba tupo pamoja, kwenye mitandao kuna mambo mengi kuanzia alivyokuwa mjamzito walisema kakimbia mara kajificha hayo mambo yapo ila tupo pamoja yule ni baby mama wangu" amesema T Bway 360.
Wawili hao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Baby Sky, ambapo T Bway amesema tangu amekuwa baba amegundua kuwa madem wamezidi kuongezeka na kumpenda kwa kumuona kama baba bora.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video