Ijumaa , 16th Jun , 2023

Viongozi wa Afrika wapo nchini  Ukraine katika ujumbe wa amani ambapo wanatarajiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky.

Viongozi saba wa Afrika, kutoka nchi kama Afrika Kusini na Misri, wataelekea Urusi hadi kesho. Kundi hilo limekubaliana kushirikiana na Zelensky na Putin juu ya usitishaji mapigano na amani ya kudumu.  Lakini mpango huo unakuja wakati Kyiv inazindua mashambulizi yake dhidi ya uvamizi wa Urusi na mapigano yanaongezeka.

Pia Ujumbe wa viongozi wa Afrika utakutana na Rais Zelensky baadaye leo kabla ya kufanya mkutano na vyombo vya habari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa lugha ya Kiingereza akisema mashambulizi ya Urusi yaliyofanywa leo  yanayoilenga Kyiv, na ni ujumbe kwa viongozi wa Afrika wanaozuru Ukraine leo:

 Wakati hayo yakijiri Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza katika mkutano wa kimataifa wa kiuchumi wa St Petersburg .