Katibu Mkuu wa CCM daniel Chongolo
Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi Kijiji cha Wenda jimbo la Kalenga mkoani Iringa na kusema kuwa ni aibu mkoa huo kusifika kwa kutoa mabinti wa kazi za ndani.
"Iringa sio mkoa wa kupata mabinti wa kazi badala yake watafute madaktari, wauguzi ,mainjinia na mabinti wenye taaluma mbalimbali,hivyo nawaomba wananchi kuhakikisha mabinti na vijana wote wanaenda shule" amesema Katibu Mkuu Chongolo
Chongolo ameeleza kuwa historia inaonesha kuwa watu walikuwa wanatafuta mabinti wa kazi mkoani hapo kwa sababu watu wa mkoa huo ni waaminifu
"Kupitia uaminifu huo kwani hawawezi kuwa watu wenye taaluma mbalimbali waaminifu mpka wawe mabinti wa kazi? alihoji? na kusema kuwa huo uaminifu wautumie kama daraja na kufanya mambo ya msingi kwa kuwasomesha watoto vizuri," ameongeza