Jumatatu , 16th Feb , 2015

Star wa muziki Bebe Cool amejitetea kutokana na hatua yake ya kuacha kuhudhuria maziko ya baba wa hasimu wake mkubwa Bobi Wine, sababu kubwa ikiwa ni kuhofia, usalama wake na wa gari lake.

Bebe Cool

Amesema alihofia usalama wake endapo angefika nyumbani kwa msanii huyo ambapo ndipo msiba ulipokuwa umehamishiwa.

Bebe Cool amesema kuwa, alikuwa na mpango wa kuhudhuria msiba huo kutokana na ratiba ya awali ambayo ilikuwa aihusishi msiba huo kufanyika nyumbani kwa Bobi Wine, huku upande wa pili mashabiki wakiendelea kuvutana upande mmoja wakiona hatua hiyo ya Bebe ni sawa na wengine wakiona kuwa sio sawa.

Bebe amekuwa ni moja kati ya watu ambao wametuma salamu za rambirambi katika msiba huo, na licha ya uhasama ulio dhahiri kati yake na Bobi Wine, staa huyo amesema kuwa ameguswa na msiba huo kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwa marehemu na pia mahusiano mazuri yaliyopo kati yake na ndugu wengine wa Bobi.