Jumatatu , 20th Mar , 2023

 

Raia wa Afrika Kusini wanafanya maandamano dhidi ya serikali na wakimtaka Rais Cyril Ramaphosa  ajiuzulu sababu za gharama kubwa ya maisha

Raia wan chi hiyo waandamana wakimtaka Rais ajiuzulu sababu ya gharama kubwa za maisha.

Serikali imepeleka wanajeshi kusaidia kulinda miundombinu muhimu wakati wa maandamano hayo.Rais Cyril Ramaphosa amewaonya waandamanaji dhidi ya kuharibu mali au kuwadhuru watu.

Wafuasi wa chama cha upinzani cha EFF nchini humo wanasafirishwa hadi katika kumbi ambazo wanafanya maandamano ya kuipinga serikali.  

Chama hicho kimesema maandamano yake ya kufungwa kwa taifa yalilenga kumshinikiza Rais Cyril Ramaphosa kuondoka madarakani, wanamshutumu kwa ufisadi na kwa kuendesha vibaya uchumi na mgogoro wa nishati.

Serikali imeimarisha ulinzi kote nchini humo. Polisi nchini Afrika Kusini hadi sasa wamewakamata watu 87 kuhusiana na maandamano hayo. Zaidi ya wanajeshi 3,000 wamepelekwa  kusaidia kulinda miundombinu muhimu.

Zaidi ya matairi 24,000 yamekamatwa na polisi katika miji tofauti.