Alhamisi , 12th Feb , 2015

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Iringa imewafikisha mahakamani watendaji watatu wa serikali kwa makosa sita ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka..

Nje ya Mahakama ya wilaya Mufindi

waliofikishwa mahakamani ni pamoja na mkuu wa wilaya ya mufindi mkoani humo Evarista  Kalalu, mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara Mikindani Limbakisye Shimwela pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya Biharamulo mkoani Kagera Nasib Mbaga wakishitakiwa.

Washtakiwa hao waliofikishwa mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Victoria Nongwa ni pamoja na mkuu wa wilaya  Kalalu, aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mufindi, Limbakisye Shimwela ambaye kwa sasa yupo Mtwara Mikindani, aliyekuwa afisa mipango Nassib Mbaga ambaye sasa ni mkurugenzi mtendaji wa Biharamulo, mhandisi Cosmas Mduda, na mkandarasi Fredrick Msimbwa.
 
Mwendesha mashataka wa takukuru imani nitume amedai mbele ya hakimu mkazi huyo kuwa washatakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Desemba 2010 na February 2011 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa ambapo walikula njama ya kula rushwa kinyume na sheria ya TAKUKURU na sheria ya manunuzi ya umma na kuingia mkataba wa ujenzi wa vyoo, mabafu na mfumo wa maji na kusababisha halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni tatu.

Washtakiwa hao wote wamekana mashitaka hayo na wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja wakidhaminiwa na wadhamini wawili kila mmoja.