
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, alipokuwa akizungumza na mamia ya waajiri na wafanyakazi walioshiriki katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).
Bonanza hilo lilowashirikisha waajiri zaidi ya 100 limefanyika katika viwanja vya Leadres Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo timu za waajiri zilishindana katika michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mbio fupi, kuvuta Kamba, kufukuza kuku na kukimbia kwenye magunia.
Aidha, Waziri Ndalichako amewakumbusha waajiri kuweka mifumo madhubuti ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuwakinga wafanyakazi na vihatarishi vya magonjwa na ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu au kuwasababishia ulemavu.
“Ninawapongeza sana waajiri wote ambao wameitikia wito wa ATE na kujitokeza kwenye bonanza hili kwa wingi kwani mwitikio umekuwa mkubwa sana hivyo nawasisitiza kwamba programu kama hizi kuwa endelevu,” amesema Waziri Ndalichako,
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba, amesema lengo la kuandaa bonanza hilo ni kuwahamasisha waajiri kuona umuhimu wa kuwekeza katika afya za wafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini.