Jumatano , 4th Feb , 2015

Msanii Ney wa Mitego amewataka mashabiki wake kufahamu juu ya ujio wa rekodi yake kali kabisa, ikiwa ni kolabo na msanii mkubwa kutoka nje ya nchi ambaye amesema kuwa kumtaja sasa si busara mpaka akamilishe baadhi ya mambo.

Msani wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego

Ney amesema kuwa anaamini kazi hii itapeleka muziki wa Tanzania mbali.

Mpaka sasa kazi hii imekwishakamilika ikiwa na ladha kutoka Afrika Kusini, Nigeria na hapa Tanzania ambapo imeguswa pia na watayarishaji kutoka ndani na nje ya nchi kama ambavyo anaeleza mwenyewe hapa.