
Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.
Aidha, Majaliwa ametembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar ambapo amemshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano.