
Wafanyabishara wakiwa Mwanza
Hayo yamebainishwa na na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala wakati akizindua Saccoss ya SHIUMA Ilemela ya wafanyabiashara wadogo ikilenga kuwezesha kundi hilo kupata mitaji yenye masharti nafuu.
Kwa upande wao wafanyabiasha hao wadogo wameeleza uanzishwaji wa Saccos ya SHIUMA Ilemela kwamba utawasaidia kufikia malengo yao ya kibiashara pamoja na kutoa wito kwa wengine kujiunga.
Aidha akifafanua kuhusu kundi hilo kurejea barabarani Mwenyekiti wa Shirikisho la wamachinga Mkoa wa Mwanza Mohamed Dauda amesema ushirikishwaji katika maeneo wanayo pelekwa ndio suluhisho.